Picha 8 mkuu wa mkoa wa Rukwa akabidhi vitanda vya kujifungulia 16, vitanda vya wagonjwa 80, magodoro 80 pamoja na mashuka 200.


Katika kuendeleza dhana ya maendeleo hayana chama Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amewashirikisha madiwani wa chama cha CHADEMA katika harambee ya ghafla iliyolenga kumalizia ujenzi wa jengo la huduma za afya ya uzazi na mtoto katika kituo cha afya Mazwi, Manispaa ya Sumbawanga.

Harambee hiyo imefanyika muda mfupi kabla ya Mh. Zelote Kukabidhi jumla ya vitanda vya kujifungulia 16, vitanda vya wagonjwa 80, magodoro 80 pamoja na mashuka 200 kwa wakuu wa wilaya ikiwa ni sehemu ya mgawo wa vifaa hivyo uliofanyika nchi nzima kupitia juhudi za Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kuimarisha huduma za uzazi nchini.

Akikabidhi vitanda hivyo kwa wakuu wa wilaya za sumbawanga,nkasi na kalambo ili nao wakavigawe katika vituo vya afya mkuu wa mkoa wa Rukwa ametumia fulsa hiyo kutoa onyo kwa baadhi ya watendaji wa idara za Afya wenye tabia zisizo endana na maadili na kazi zao.

Mganga mkuu wa mkoa wa Rukwa DR. Bonifasi Kasululu amemshukuru raisi kwa uamzi wa kupunguza changamoto zinazo ikabili huduma za wajawazito nchini shukrani zinazo tolewa pia na wadau wengine hapa sumbawanga.

Posted by peter kapola 0764033168
 









Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment