ASKARI WA USALAMA BARABARANI AGONGWA GARI BARABARANI Tuesday, July 11, 2017


Askari wa usalama barabarani "trafiki" mkoani Tabora amefariki dunia baada ya kugongwa na gari wakati akitekeleza majukumu yake. 

Askari huyo aliyefahamika kwa jina E.51 Koplo Aswile Ambwene amefariki dunia jana asubuhi ya saa 12:30 akiwa kazini eneo la barabara ya Sikonge, kijiji cha Kipalapala kwa Chief, kata ya Itetemia, mkoani Tabora.


Mauti ya askari huyo yalisababishwa na gari lenye namba za usajili 564 ALG aina ya Isuzu likiendeshwa na dereva Hasan Husein-Kiula mwenye umri wa miaka 36. Gari hilo lilikuwa likitokea Mpanda kwenda Kahama likiwa limepakia magunia ya mahindi.


Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo alieleza kuwa Bwana Hasan(dereva wa gari hilo) alisimamishwa barabarani na askari mwenye namba G.4246 Konstebo Abuu lakini dereva huyo aligoma kusimama na kusababisha kumgonga askari namba E.51 Koplo Aswile Ambwene ambaye alipoteza maisha papo hapo.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Milambo Jeshini mkoani Tabora.
Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment