WANAFUNZI 10 WAFUTIWA MATOKEO YA MTIHANI KIDATO CHA SITA 2017 Saturday, July 15, 2017



Wakati matokeo ya mtihani wa kidato cha sita yakitolewa leo, Jumamosi Julai 15, imebainika kuwa watahiniwa 10 walifutiwa matokeo kwa makosa ya kufanya udanganyifu.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Charles Msonde imeeleza kuwa kati ya watahiniwa hao kumi, saba ni wa shule na watatu ni wa kujitegemea.
Pamoja na hao kumi, matokeo ya watahiniwa wengine 15 yalizuiliwa kwa kuwa hawakufanya mitihani ya baadhi ya masomo.
Watahiniwa hao walishindwa kufanya mitihani kutokana na matatizo mbalimbali ikiwamo ya kiafya na hivyo kushindwa kufanya baadhi ya mitihani hiyo.
‘Watahiniwa hao wamepewa fursa ya kufanya mitihani ya kidato cha sita, Mei 2018 kama wa watahiniwa wa shule,” imesema taarifa ya Dk Msonde.
Pia, wapo watahiniwa 69 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mitihani yote, wamepewa fursa ya kufanya mitihani hiyo, Mei 2018.

Angalia hapa chini Matokeo hayo




Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment