Watu watatu wameuwawa kwa kuchomwa moto wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa baada ya kuiba ng’ombe 16 .

Related image 
 
WATU watatu  wameuwawa   kwa   kuchomwa  moto    katika   kijiji  cha  Mao  kata  ya  Mbuluma   wilaya   ya  Kalambo  mkoani   Rukwa  baada   ya  kuiba   ng’ombe  16    mali  ya    Mtokambali   Nsosomo .

Diwani  wa  kata  hiyo    Saidi  Manoti,  amekimbia   kituo  hiki  kuwa   wezi  hao  walikuwa  wametokea  katika  kijiji  Nchenje    wilaya  jilani  ya   Nkasi  na  kuvamiwa  katika  kijiji  cha  mao   kisha  kuchomwa  moto.

Aidha  amesema  watu  hao  hawakutambulika   majina  wala  makazi   yao  na kuwa  mpaka  sasa wanategemea  kuitisha mikutano  ya hadhara  ili   kutoa  elimu   kwa  wananchi  juu  ya  kuachana  na  vitendo  vya  kujichukulia  sheria  mkononi.

Kamanda  wa  polisi  mkoani  Rukwa  Geoge  Simba  kyando, amekiambiaa  kituo  hiki  kuwa   watu  sita  (6) wamekamatwa  na  watafikishwa  mahakamani  pindi  upelelezi  utakapo  kamilika .
 
Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment