Vitendo vya
kikatili vimeendelea kushamiri Mkoani Mbeya baada ya mwanamke mmoja (Majina
yamehifadhiwa) (31) mkazi wa Mtaa wa Mwanshinga Kata ya Maanga Jijini Mbeya
kujeruhiwa vibaya usoni na mkononi kwa kumwagiwa maji yanayodhaniwa kuwa na
tindikali na mtu asiyejulikana kutokana
na wivu wakimapenzi.
Akiongea kwa
taabu akiwa wodi namba mbili katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya mhanga wa
tukio hili amesema kuwa tukio hilo limetokea Julai 19 mwaka huu majira ya saa
tatu na dakika arobaini na tano alipokuwa anarejea nyumbani akitokea kwenye
shughuli zake.
Aidha
amesema katika mkasa huo alijeruhiwa yeye na wanawe wawili wa kike (majina
yamehifadhiwa)Loveness Peter(11)mwanafunzi wa darasa la sita ambaye naye
amelazwa katika Hospitali ya Rufaa na Nancy Peter(5)ambaye ametibiwa na
kuruhusiwa.
Amesema
chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi ambapo amesema kuwa amemtambua
aliyefanya tukio hilo amemtambua kwa jina moja la Emma jinsi ya kike ambapo
amesema mtuhumiwa mara kadhaa alimtishia kuwa atamfanyizia.
Kwa upande
wao Madaktari wadi na mbili Daktari Margaret Kimwaga,Daktari Joseph Konyo na
Daktari John Steven wamesema hali ya mgonjwa imeanza kuimarika tofauti na
alivyopokelewa.
Naye Mkuu wa
Dawati la Jinsia Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya Janeth Masangano amesema Dawati
lake linafuatilia kwa kina juu ya tukio hili ili kumbaini alyehusika na kutoa
wito kwa watu kuacha kujichukulia sheria mkononi.
0 comments:
Post a Comment