WATU wawili
wafamilia moja wamefariki
dunia katika kijiji
na kata ya
Kisumba tarafa ya
kasanga wilaya ya
Kalambo mkoani Rukwa na wengine 6 wamelazwa
baada ya kula
ugali wa muhogo.
Diwani wa
kata hiyo Inosent
Kukongwa , alisema watu
hao ambao ni
wafamilia moja walikula
ugali wa muhogo ambao ulikuwa
umeandaliwa kama chakula
cha usiku , ambapo
baada ya kula
walianza kuharisha na
kupelekea watoto wawili
kufariki dunia na wengine sita
kumbizwa zahanati kwa
matibabu zaidi.
Amesema baada
ya kutumia chakula
hicho waliamua kutumia
dawa ya kienyeji
badara ya kwenda
hospitali na kupelekea maafa
ya watoto hao.
‘’Inasikitisha
kwani
baada ya kula
chala hicho hawakutaka
kwenda zahanati na
badara yake waliendelea
kujitibu kwa kutumia miti shamba
na kushituka baada
ya kuona hali
bado ilikuwa ikiendelea
kuwa mbaya’’alisema kukongwa.
alisema baada
ya tukio hilo kutokea
waliamua kutoa taarifa
kwenye uongozi wa
wilaya na kwa
jeshi la polisi , ambapo
kwa pamoja walifika
eneo la tukio
kisha kushuhudia uwepo
wa tukio hilo.
Afisa tarafa
ya kasanga Peter
Mankambila , ambae licha ya
kukili wazi kutokea
tukio hilo ,alisema baada
ya kupata taarifa
alimua kuelekea eneo
la tukio na kubaini
watoto hao kufariki
kwa kula chakula
cha ugali wa muhogo.
Alisema watu
watu sita wanaendelea
kupatiwa matibabu kwenye
zahanati ya kiijiji
hicho .alisema kwa
kawaida ugali wa muhogo
huliwa maara baada
ya kuolowekwa kwa
zaidi ya siku
tatu .
Alisema lakini
inaonyesha familia hiyo
ili kula ugari
huo bila kuoloweka
vizuri kwani muhogo
unaolimwa kwenye maeneo
hayo huwa ni
mchungu kupita kawaida
hivyo bila kuoloweka
vizuri ni lazima
ukuletee madhara kiafya kama ilivyo
tokea kwa familia
hiyo.
Alisema katika
eneo la mwambao
wa ziwa tanyika watu
hulima kilimo cha
muhogo kwa asilimia
kubwa ukilinganisha na
maeneo mengine, ambapo
wakisha lima
na kutoa mashambani
huanika kisha kuoloweka
kwa zaidi ya
siku tatu na
kusaga tayari kwa
chakula.
Kamanda wa
polisi mkoani Rukwa
Geoge Simba Kyando
, ambae licha ya
kukili kutokea tukio
hilo, alisema kuna taarifa
mkanganyiko juu ya tukio hilo na
kuahidi kutoa taarifa
zaidi mara baada
ya uchunguzi kukamilika.
‘’kuna taarifa
mkanganyiko kwenye tukio hili
kwani inadaiwa kuwa
familia hiyo ilitumia
dawa ya kienyeji
na zingine zinadai kuwa
walitumia ugari wa
muhogo hivyo tunashindwa
kupata taarifa sahihi ni
zipi hivyo nafikiri nitatoa taarifa
zaidi uchunguzi ukikamilika
na kubaini chanzo
halisia cha vifo
vya watu hao.’’alisema
kamanda kyando.
0 comments:
Post a Comment