ERIKALI katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa imepiga marufuku wananchi kulima kilimo cha fuga kwenye vyanzo vya maji na kuwa itachukua hatua kali za kisheria dhidi ya viongozi wa serikali za vijiji na kata ambao watafumbia macho swala hilo.
Hatua hiyo inakuja baada ya wananchi wilayani humo kuharibu vyanzo vya maji kwa kulima kilimo cha fuga , ambacho hulimwa wakati wa msimu wa kiangazi , ambapo wananchi hulima kilimo hicho pindi maji na mito inapo kauka kwenye mikondo yake na kutumia unyevu huo kujipatia mazao wakati wa msimu wa kiangazi.
Mkuu wa wilaya hiyo Julith Binyura ,amekiambia kituo hiki kuwa wananchi wanapaswa kulima umbali wa mita sitini 60 kutoka usawa wa vyanzo vya maji kwa lengo la kuepukana na kukauka kwa vyanzo vya maji sambamba na kujitokeza kwa ukame kwenye maeneo husika.
Aidha Binyura amewataka wananchi kuacha tabia ya kuchoma misitu kiholela na kuwa atakae bainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Amesema serikali itachukua hatua kali kwa viongozi wa serikali za vijiji ambao wataoneka wakifumbia macho swala hilo .
0 comments:
Post a Comment