WATU watano wakiwemo watoto wawili
wamekufa katika matukio tofauti yaliyotokea mkoani ambapo mganga wa
jadi, Levocatus Kanjalanga (65) ameuawa kikatili kwa kuchomwa mkuki
mgongoni na mtu asiyefahamika.
Matukio hayo ambayo yametokea katika
Wilaya za Nkasi, Kalambo na Manispaa ya Sumbawanga yamethibitishwa kwa
nyakati tofauti na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, George Kyando na
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Wilaya, Said Mtanda.
Mtoto wa mganga huyo, Simon Kanjalanga
alilieleza kuwa baba yake aliuawa juzi saa moja na nusu asubuhi kwa
kupigwa na mkuki mgongoni akiwa anatembea mitaani katika kitongoji cha
Chawe kilichopo katika Mji wa Namanyere wilayani Nkasi.
Taarifa kutoka eneo hilo la tukio
zinaeleza kuwa mganga huyo wa kienyeji alikuwa akituhumiwa na wateja
wake kuwa alikuwa akiwatoza fedha nyingi za matibabu lakini walikuwa
hawaponi kupitia uganga wake huo.
Akithibitisha Mkuu wa Wilaya hiyo,
Mtanda alieleza kuwa watu wawili wameuawa kikatili wilayani humo akiwemo
mganga huyo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni imani za kishirikina .
Duh
ReplyDelete