Watu
sita wanaosadikiwa kuwa majambazi wameua katika majibizano ya risasi na
polisi katika mtaa wa Fumagila Mashariki Kata ya Igoma jijini Mwanza.
Tukio
hilo lilitokea usiku wa kuamkia leo baada ya watu hao kuzingirwa
katikati ya majengo mtaani hapo na kufanya mashambulizi ya kujibizana
risasi kwa muda mrefu.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo lakini akaomba alitolee ufafanuzi baadaye kwa kuwa hivi sasa bado
anaendelea kukusanya taarifa zaidi.
“Ni
kweli hilo tukio hilo lipo, ila bado tunashughulikia naomba munipe muda
nitataoa ufafanuzi baadaye,” alisema kwa ufupi Kamanda Msangi.
Shuhuda
wa tukio hilo, ambaye ni diwani wa Kata ya Kishili iliyo jirani na kata
hiyo, Sospeter Ndumi amesema kurushiana risasi baina ya watu hao na
polisi kulianza usiku wa manane hadi majira ya asubuhi.
Amesema
katika majibizano hayo polisi walifanikiwa kuwaua watu hao na kukamata
silaha mbalimbali za kivita walizokuwa wanazitumia.
Katika
mtaa huo huo ndipo lilipotokea tukio la Desemba 3 mwaka jana ambapo
polisi waliwakamata watoto 11 wenye umri unaokadiriwa kuwa na miaka sita
hadi 14 baada ya kuizingira nyumba moja kwa lengo la kuwakamata watu
waliowahisi kuwa majambazi.
Mmoja
kati ya watu watatu waliokutwa kwenye nyumba hiyo alikimbia baada ya
kuwarushia polisi bumu la mkono, kabla ya polisi kuwadhibiti waliosalia
kwa kushirikiana na wananchi wa mtaa huo.
Kadhalika
katika tukio hilo, watu watatu waliosadikiwa kuwa ni majambazi waliuawa
na bunduki mbili aina ya SMG na AK47, magazine saba, bastola moja na
risasi 183 vilikamatwa na polisi.
Baada ya polisi kuondoka katika eneo hilo, wananchi waliiteketeza nyumba hiyo kwa moto.
0 comments:
Post a Comment