Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Magufuli jana alisali Ibada
ya Jumapili ya 15 ya mwaka wa Kanisa iliyofanyika katika Kanisa la
Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita na kuendesha harambee ya
kuchangia ujenzi wa kanisa hilo.
Katika harambee hiyo Mhe. Rais Magufuli ambaye aliongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli alifanikiwa kuchangisha fedha taslimu kiasi cha Shilingi Milioni 13, ahadi Shilingi 920,000/=, mifuko ya saruji 33 na malori 2 ya mchanga.
Mhe.
Rais Magufuli aliwapongeza waumini wa Parokia ya Chato kwa hatua kubwa
waliyopiga katika ujenzi wa kanisa kuu la Parokia hiyo na amewataka
kuendelea kujitolea kukamilisha hatua za mwisho za ujenzi huo.
0 comments:
Post a Comment