Monday, July 17, 2017 Polepole: Tuna orodha ndefu ya viongozi wa upinzani wanaotaka kuhamia CCM.




Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Humphrey Polepole amesema anayo orodha ndefu ya viongozi wa upinzani wanaotaka kuhamia CCM.

Polepole alisema hayo jana huku akibainisha kuwa orodha hiyo inahusisha wenyeviti, madiwani na wabunge lakini siku nyingi tu alikuwa amewakatalia kuwapokea.

Hata hivyo Polepole alisema kwamba kutokana na kutuhumiwa kuwanunua sasa anafanya kweli, atawachukua mmoja mmoja.

Polepole alisema amemua kuchukua uamuzi huo baada ya Chadema kuonyesha utovu wa nidhamu kwa kudai kuwa madiwani wanaokihama chama hicho wamehongwa na CCM.

“Sasa tutaanza kumchomoa mmoja baada ya mwingine na kwa kutekeleza hilo wiki hii watampokea kiongozi mkubwa wa chama hicho,’’anasema Polepole.

Alibainisha kuwa kama chama kinakuwa na viongozi wanaoweza kuhongwa na wakahongeka basi  chama hicho kitakuwa ni cha hovyo
 
"Madiwani wamesema wanamuunga mkono John Magufuli, wametoka wenyewe wameanza kusema CCM imewanunua, sasa kwa vile wameanza utovu wa nidhamu nitaanza kumtoa mmoja baada ya mwingine,’’anasema.

Polepople anaongeza kwamba: “Nilikua nakataa kuwapokea ila nina orodha kubwa wapo wenyeviti, wabunge kibao kama vile watu wanaojisaliji kodi ya majengo TRA"
 
"Unajua wanasema wanaisoma namba, nawahakikishia baada ya miaka mitano kwa spidi hii iliyoanza nayo CCM namba inayoonekana wakati huu itakuwa haisomeki kabisa, nitafanya shoo ndogo tu kuwachomoa viongozi hao sipendi kwenda kuwachukua wengi sababu nitaonekana kama nawahujumu vile na pia ili upinzani usikose watu angalau wa kuzungumza nao,"alisema

Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment