13 hours ago
MCHANGANYIKO
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa pili kushoto) akitoa maelekezo
kwa Mkandarasi anayejenga Kituo cha Mzani cha Singiwe Kilichopo katika
barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga Port (112KM) Mkoani Rukwa wakati
alipokagua ujenzi huo Mkoani Rukwa.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Katikati) akipanda katika Daraja la
Mto Kalambo Mkoani Rukwa wakati alipokagua daraja hilo ambalo ujenzi
wake umekamilika.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa pili kulia) akikagua Daraja la
Mto Kalambo Mkoani Rukwa wakati alipokagua daraja hilo ambalo ujenzi
wake umekamilika.Wa kwanza ni Meneja wa Wakala wa barabara (TANROADS)
Rukwa Eng. Msuka Mkina
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa pili) akielekeza jambo kwa
Msimamizi wa bandari ya Kigoma,Bw. Morris Mchindiuza (Wa kwanza) wakati
alipokagua huduma za bandari ya Katanga Mkoani Rukwa.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa pili kulia) akipokea taarifa ya
ujenzi ya barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasnga Port (112KM) Mkoani Rukwa
wakati alipokagua ujenzi huo Mkoani Rukwa.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (aliyenyoosha kidole) akiongea na
wakazi wa kijiji cha Katete Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa wakati
alipokagua barabara ya Matei-Kasesya (KM).
………………………………………………………………………………….
Serikali kupitia Wakala wa
barabara nchini TANROADS mkoa wa Rukwa imekamilisha ahadi yake kwa
wananchi ya kuwapunguzia changamoto ya usafirishaji wa abiria na mzigio
kwa kukamilisha ujenzi wa Daraja la mto Kalambo pamoja na barabara ya
Sumbawanga Matai hadi Kasanga port (112km) ambapo Kilomita 71.4
zimeshawekwa lami.
Akizungumza mara baada ya kukagua
daraja na barabara hiyo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng.
Edwin Ngonyani amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutafungua fursa za
kiuchumi kwa wananchi wa mkoa Rukwa na nchi nyingine za jirani ikiwemo
Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi.
“Tuliwaahidi wananchi kujenga
darala na barabara hii ili wafanyabiashara na wakulima waweze
kusafirisha bidhaa na mazao yao kwenda katika masoko kwa wakati na hivyo
kukuza uchumi wao binafsi na taifa kwa ujumla,” ameaema Eng. Ngonyani.
Ameongeza kuwa chini ya uongozi
wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli Serikali itahakikisha ndani ya kipindi
cha miaka mitano inakamilisha ahadi zote walizoahidi kwa wananchi ili
wananchi wanufaike na Serikali yao.
“Serikali ya Dkt. John Pombe
Magufuli ipo kwa ajili ya wananchi wote, na sisi kama wasimamizi
tuliopewa dhamana kwenye Wizara tutahakikisha kile tulichokiahidi kwa
wananchi tunakitekeleza kwa wakati ili wananchi wanufaike na uchumi wa
nchi ukue,” amesisitiza Eng. Ngonyani.
Kwa upande wake Meneja wa
Tanroads Rukwa amewataka wananchi kutunza miundombinu ya barabara na
kuacha vitendo vya kung’oa alama za barabarani ambazo zimewekwa ili
kuongeza usalama kwa madereva katika matumizi ya barabara hizo.
“Tumeweka alama hizi barabarani
kwa ajili ya kuongoza madereva wanaotumia barabara ili kuepusha ajali
zinazoweza kutokea kwa kutokuwepo na alama za tahadhari, hivyo ni wajibu
wenu kuzilinda na kuzitunza kwani zipo kwa faida yetu sote,” amesema
Eng. Msuka Mkina
Katika hatua nyingine Waziri
Ngonyani amekagua huduma za bandari ya Katanga ambapo amesema Serikali
itaendelea kuziboresha bandari zilizopo ukanda wa ziwa Tanganyika ili
kuvutia wasafirishaji wa mizigo mikubwa kutumia bandari hizo.
“Tutaendelea kuimarisha
miundombinu ya bandari ya Kalema, Kigoma na Katanga ili ziwe na uwezo wa
kupakia na kupakua mizigo mikubwa kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC) na Burundi,” amesisitiza Eng. Ngonyani.
Naye Msimamizi wa Bandari Mkoa wa
kigoma, Bw. Morris Mchindiuza amesema Mamlaka ya bandari TPA imejipanga
na imetenga kwenye bajeti yake kiasi cha Sh. bilioni 1 kwa ajili ya
upanuzi wa Gati namba moja na hivyo kuchochoa ukuaji wa wa kibiashara na
ongezeko la Meli hususani nchi za jirani kama Burundi na DRC Congo.
Naibu Waziri Eng. Ngonyani yupo
katika Ziara ya kukagua Miundombinu ya barabara, Viwanja vya Ndege,
Ujenzi wa Nyumba za viongozi, huduma za mawasiliano ya simu, Bandari
na Madaraja katika Mkoa wa Rukwa
0 comments:
Post a Comment