Friday, July 14, 2017 Ofisi ya CCM Yachomwa Moto Pwani


Watu wasiojulikana wameichoma moto ofisi ya Chama cha Mapinduzi tawi la Mshonzini iliyopo wilayani Mafia mkoani Pwani na kuteketeza mali mbalimbali za chama hicho.

Akithibitisha tukio hilo, Katibu wa CCM wilayani Mafia Mohammed Dhikiri amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana  Alhamisi Julai 13.

Dhikiri amesema moto huo umeteketeza kabisa ofisi hiyo pamoja na samani za ndani.

Amesema bado haijajulikana sababu za ofisi hiyo kuchomwa moto kwa kuwa wakati tukio linatokea hakukuwepo na viashiria vyovyote vya vurugu miongoni mwa wanachama.

Amesema bado halijafahamika ni nani aliyehusika na tukio hilo na kueleza kuwa wameliachia Jeshi la Polisi kuendelea na uchunguzi zaidi dhidi ya tukio hilo.

Naye  Mbunge wa Mafia, Mbaraka Dau amesema vipo viashiria vinavyoonyesha kuwa alifika mtu asiyejulikana karibu na ofisi hiyo kisha kuwasha na kurusha kijinga cha moto kwenye paa la makuti la ofisi hiyo.

Dau amesema mtu huyo baada ya kutekeleza kitendo hicho aliondoka kuelekea kichakani kama ambavyo alama za nyayo za miguu yake zilivyoonyesha.

Amesema hilo ni tukio la kwanza kutokea wilayani humo kwa kuwa hadi linatokea hapakuwa na viashiria vyovyote vile vya kutokuwepo kwa Amani kati ya wanachama au viongozi.

Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment