Mtu mmoja mkazi wa kata ya
mafulala mtaa wa sekondari Anna
Kashamakula (40) ameuawa kwa kuchomwa na kisu na mume wake katika manispaa
ya sumbawanga mkoani rukwa.
Tukio hilo la kushangaza limetokea usiku wa kuamkia
leo majira ya saa sita usiku baaba ya kutokea ugonvi wa kifamilia kwa wawili
hao na hivyo kupelekea mume wa marehemu kuchukua uamzi wa kumchoma mke wake
kisu kisha kitoweka pasipo kujulikana.
Hata hivyo akizungumza kwa
majonzi moja kati ya mtoto wa marehemu huyo ameeleza kuwa chanzo cha tukio hilo ni kuto kuelewana
kwa wazazi hao wawili kwa mda mrefu.
Kwa upande wao baadhi ya
wananchi ambao walikuwa mashuuda wa tukio hilo
wamesema kuwa chanzo cha tukio hilo
ni kutokana na mume huyo kutumia kiasi cha pesa alichopewa na marehemu kwaajili
ya kulipia pango na hivyo kushindwa kutekelerza na kuamua kufanya ukatili huo.
Nae mwenyekiti wa mtaa huo wa
sekondari Christopha Kalinji amesikitishwa kutokea kwa tukio hilo na hivyo kuwataka wananchi kuonesha
ushilikiano ili kumtafuta mtuhumiwa popote alipo ili aweze kuchukuliwa hatua za
kisheria.
Kamanda wa polisi mkoani Rukwa
kamishna mstaafu George simba Kyando amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa upeleleza
bado unaendelea ili kuweza kuakikisha mtuhumiwa anafishwa katika vyombo vya
dola sambamba na kuwataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi.
0 comments:
Post a Comment