Mtoto aliyekanyagwa na gari enzi za uhai wake
Habari
zilizotufikia hivi punde katika chumba cha habari cha Malunde1 blog ni
kwamba mtoto wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa mwaka mmoja
amefariki dunia papo hapo leo usiku Jumatatu Julai 24,2017 baada ya
kukanyagwa na gari wakati dereva akirudisha gari lake nyuma bila
kuchukua tahadhari.
Tukio hilo limetokea usiku huu nyumbani
kwao na mtoto huyo katika mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi katika
manispaa ya Shinyanga.
Kwa Mujibu wa mwenyekiti wa mtaa huo na kata hiyo,David Nkulila amesema
mtoto huyo amekanyagwa na gari hilo linalodaiwa kuwa ni la serikali
nyumbani kwao.
Imeandikwa kila nafsi itaonja umauti
ReplyDelete