Zikiwa zimesalia siku chache kuelekekea uchaguzi mkuu wa serikali za mitaa hapa nchini , watendaji wa serikali za vijiji na kata zinazopokana na nchi jilani ya Zambia wilayani Kalambo mkoani Rukwa wametakiwa kuwa makini na kuhakikisha wahamiaji wote wanaongia nchini kinyemera na kuanzisha makazi hawashiriki zoezi hilo.
Kumekwepo na changamoto ya baadhi ya raia kutoka nchi jilani ya Zambia kuingia nchini kinyemera na kuchukua kadi za kupigia kura na kuzitumia katika mambo mbalimbali ikiwemo kupiga kura na kujitambulisha kuwa ni watanzania.
Kwa kulitambua hilo katibu tawala wilayani kalambo Frank Schalwe amekaa kikao na watumishi wa umma kilichoketi katika tarafa ya Mambwenkoswe wilayani humo , amesema zaidi ya wananchi elfu themanini na tisa wamejitindikisha kwenye daftari la wapiga kula hivyo wanapaswa kuhamishwa ili waweze kuwachagua viongozi wanaowataka kauli iliungwa mkono na afisa tarafa ya Mambwe Nkoswe Mpapalika mfaume.
Baadhi ya watumishi wa wilayani humo wamesema wamejipanga kudhibi wahamaji kuto kupiga kura wakati wa zoezi husika.
Kituo hiki kimkutana na baadhi ya raia wa Zambia wanaishi mpakani mwanchi ya Tanzania na Zambia wamesema sisi ni wamoja hivyo wazambia hawapaswi kuingilia uchaguzi wa Tanzania.
Na peter kepola
0 comments:
Post a Comment