MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Tanga katika kusherehekea miaka 20 wamekabidhi zawadi ya mashuka 80 katika kituo cha Afya Pongwe kilichopo Kata ya Pongwe Jijini Tanga.
Akizungumza wakati akipokea mashuka hayo Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa aliwataka wananchi kuchangamkia fursa za kujiunga na Bima ya Afya ili kuweza kupata uhakika wa kupata matibabu kutokana na kwamba siku zote magonjwa hayabishi hodi yanapokuja .
Alisema kwa sababu huja muda wowote hivyo ni muhimu waweze kuwa na bima ya afya kwani wakifanya hivyo watakuwa wamejitengenezea utaratibu wa uhakika wa matibabu kwa mwaka mzima na kuondosha changamoto ambazo wangekumbana nazo.
“Kwanza niwashukuru NHIF kwa namna mlivyoonyesha umuhimu kwenye sekta ya afya na kuamua kutoa msaada huo na niwaombe muendelee kutusaidia katika kuhakikisha tunamaliza changamoto mbalimbali zilizopo”Alisema
Alisema duniani kote moja ya jambo muhimu la kuwekeza kuliko chochote ni sekta ya afya kutokana na wao wenyewe ni watanzania mazingira yao wanayajua na maisha yao na magonjwa hayapigi hodi yanakuja siku ambayo ukiwa hauna fedha.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kutokana na hilo Serikali ikaona kuna kila sababu ya kufikia hatua kila mtanzania kuwa na bima ya afya ili kuweza kupata matibabu.
“Serikali imeona kuna sababu ifike hatua iwe ni sheria kila mtanzania anapozaliwa ana miliki bima ya afya ili aweze uhakika kupata matibabu kutokana na kwamba fedha haitunziki na matatizo yanakuja pale kwenye changamoto”Alisema
Alisema sasa inaweza kutokea unapata shida unapokwenda hospitali huna fedha na kupelekea kukaa nyumbani na mgonjwa wako na hivyo kupelekea kupoteza maisha.
“Niwapongeze NHIF na niwaombe wananchi maisha yetu tunayajua na sisi tunaotegemea shughuli za kilimo fedha zetu ni za msimu kutokana na wakati mwengine hatuna sasa kama tutajenga utamaduni ya kujiunga na mpango huo utatusaidia kupata matibabu “Alisema DC Mgandilwa.
Awali akizungumza wakati wa sherehe hizo,Meneja wa NHIF Ally Mwakababu alisema katika miaka 20 mfuko huo umepitia hatua mbalimbali na wameamua kutoa msaada huo kituo cha Afya Pongwe kwa sababu ya idadi ya watu wanaohudumiwa eneo hilo na uhitaji.
Alisema mfuko huo umeamua kurudisha kidogo kwa wananchi na wametoa mashuka ili kuwawezesha wagonjwa kuweza kulala mahali pazuri na kupata huduma bora.
“Pongwe inahudumia kata mbili na baadhi ya wilaya nyengine hivyo tunatamani watu wapate mahali pazuri na tunajivunia miaka 20 ya NHIF mfuko mkoa wa Tanga huduma zimeimarika na wameweza kuboresha huduma mbalimbali”Alisema
Alisema huduma hizo ni pamoja na kutoa mikopo kwa vituo,mikopo ya ukarabati na ununuzi na vifaa tiba na kulipa kwa wakati madai ya wanachama wanaotibiwa na vituo hivyo na hivi sasa NHIF tumeingia kwenye mfuko wa Kidigitali”Alisema .
Naye kwa upande wake Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga (CMO) Dkt Charles Mkombe alishukuru kwa msaada huo wa mashuka 80 ambao wameupata kutoka kwa wadau wao NHIF.
Alisema kwa kiasi kikubwa kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya kuna changamoto nyingi wanazokutana nazo hasa bidhaa za afya na shirikishi kwenye kutuo huduma na mashuka ni bidhaa muhimu kwa maisha ya wagonjwa wanaolazwa .
“Niwashukuru NHIF kwa maada huu mkubwa kwani tuna upunguza vifaa mbalimbali ikiwemo mashuka ambayo yanatumika kwenye vitu vikubwa na bado tunaupungufu wa mashuka watakaoguswa wajitokeze watuwasaidie”Alisema
0 comments:
Post a Comment