Songwe, February 21.2023
Wananchi mikoa ya Mbeya na Songwe Wametakiwa kujikita katika kilimo Cha mazao ya Kibiashara Ili kujikwamua kiuchumi.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa kiwanda Cha kuzalisha Unga lishe kutoka Kampuni ya Amaranth Ndg. Pendo Patrick Kilichopo Eneo la nane nane mkoani Mbeya wakati akifanya ukaguzi wa Mashamba ya viazi na mahindi lishe yaliyopo wilayani Momba mkoani Songwe.
Pamoja na hayo amesisitiza wakulima kujikita katika kilimo Cha Aina tofauti tofauti hasa katika mazao ya Kibiashara hasa Kwa vijana Ili kupambana na tabia ya baadhi Yao kuwa tegemezi na kuishia kulalamika kuwa maisha ni magumu angali wanashindwa kujituma na wengi wao kukimbia shughuli za shambani na kuishia kulalamikia serikali.
Picha. Baadhi ya wafanya kazi wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wao Momba Songwe shambani.
Hata hivyo Kampuni hiyo mpaka Sasa imeendelea kuajiri vijana katika Kampuni hiyo ya Kuzalisha Unga lishe mkoani Mbeya sambamba na wananchi mbalimbali wanao pata fulsa katika Mashamba ya viazi na mahindi lishe yaliyopo wilayani Momba Mkoani Songwe ambapo mpaka Sasa zaidi ya wafanya kazi 100 wameajiriwa kupitia Kampuni hiyo.
Picha ya baadhi ya wafanya kazi wa shambani wakiweka mbolea kwenye Moja ya Mashamba lishe ya mahindi.Pamoja na hayo Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ndg. Pendo Patrick, Anaendelea kuwashukuru baadhi ya wadhamini wanao Unga mkono jitihada mbalimbali katika kiwanda hicho ikiwa ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Bank ya CRDB Mbeya, Kampuni ya Hervetazi na Kibowavi na wafanya kazi wote anao shirikiana nao katika majukumu ya kikazi.
Picha. Muonekano wa shamba la viazi lishe Momba Songwe.
Picha. Maendeleo ya shamba la viazi lishe wilayani Momba mkoani Songwe.
0 comments:
Post a Comment