MKAZI
mmoja wa kijiji cha Kateka kata ya matai wilaya ya
kalambo mkoani Rukwa Geradi konza mwenye umri wa miaka {70}
ameuwawa kwa kukatwa na mapanga katika sehemu mbalimbali za
mwili wake na mtu au watu wasio fahamika kisha mwili wake
kutupwa mashmabani.
Afisa
tarafa ya matai Edrue Ngindo, amekiambia kituo hiki kuwa
tukio hilo la kushangaza na la kusitisha limegundulika
kupitia wafugaji ambao walipita maeneo ya mashamba yaliopo
eneo la katete mpkani na kijiji cha kisungamile na kumkuta
mzee huyo akiwa ameuwawa.
Ambapo
baada ya kupata taarifa walimua kuelekea eneo la tukio na
kukuta marehemu akiwa ameuwawa kwa kukatwa na mapanga na kuwa
chanzo cha tukio bado hakija fahamika na juhudi za
kuwatafuta wahusika watukio hilo bado zinaendelea .
Aidha
Ngindo amesema Jeshi la polisi lilifika eneo la tukio kisha
kuukabidhi mwili wa marehemu kwa ndugu tayari kwa mazishi
na kuwataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria
mkononi kwani ni kosa kisheria.
Hata
hivyo juhudi na maalifa za kumtafuta kamanda wa polisi
mkoani Rukwa Geoge Simba kyando zimegonga mwamba baada ya
simu yake kuita bila kupokelewa.
0 comments:
Post a Comment