VIONGOZI WA DINI WANAOPENDA SANA SADAKA WAONYWA


KANISA la Moravian la Uamsho Tanzania limekemea baadhi ya viongozi wa kidini wanaojipendekeza kwa watu wenye fedha kwa kutaka kuwaombea ili wapate sadaka nono.

Aidha, kanisa hilo limeungana na makanisa ya Uamsho ya Moravian Marekani na duniani kote, kutoa tamko rasmi la kupinga ushoga na usagaji na kuweka bayana kuwa halitafungisha ndoa za jinsi moja.

Askofu Mkuu wa kanisa hilo Tanzania, Emmaus Mwamakula aliyasema hayo hivi karibuni katika Ibada ya kuwasimika wachungaji mashemasi na makasisi wa kanisa hilo iliyofanyika katika kanisa la Mbweni, Dayosisi Kuu ya Dar es Salaam.

Akizungumza katika ibada hiyo, Askofu Mwamakula alisema utumishi wa Mungu katika dunia hii umewekwa kwa kusudi la kuleta amani, furaha na umoja katika jamii, kusaidia waliotindikiwa imani kumkaribia Mungu zaidi na si kujinufaisha wenyewe.
Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment