Mkazi mmoja wa kijiji cha Kafukoka kata ya Kisumba wilaya ya kalambo mkoani Rukwa kalasto katanti miaka 40 ameuwawa kwa kuchalazwa na bakora katika sehemu mbalimbali za mwili wake na ndugu zake baada ya kushindwa kulipa deni la shilingi elfu sitini na nne (64000).
Tukio hilo la kusikitisha limetokea baada ya kujitokeza ugovi mkali baina ya ndgu hao, ambapo kufumba na kufumbua kijana huyo bila kujua hili wala lile masikini ya mungu alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuchalazwa bakora katika sehemu mbalimbali za mwili wake na kupelekea kifo chake hapo papo.
Kutokana na kilio kusikika maeneo hayo watu kutoka sehemu mbalimbali walikusanyika eneo la tukio na kutoa taarifa kwenye ungozi wa kijiji hicho ambao ulitoa taarifa polisi ambao walifika mapema na kuluhusu ndugu kufanya mazishi baada ya uchunguzi kukamilika.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo katibu tawala wilayani humo Frank sichalwe amesema watu wawili wanashikiliwa na jeshi la polis wilayani humo akiwemo Florensi Zunda na Dafusi Zunda, na kuwataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi.
Posted by kapola newz.com.
0 comments:
Post a Comment