Mtoto mwenye umri wa miaka 13 mkazi wa kijiji cha santamalia kata ya Matai wilayani Kalambo mkoani Rukwa Benedkti Salum amefariki dunia kupigwa kwa ngumi na mateke na baba yake mzazi kutokana na ulevi wa kupindukia.
Wakiongea kwa masiko makubwa huku wakilia kwa uchungu mkubwa ndugu wa mtoto huyo akiwemo mama mzazi wa mtoto huyo Hilda Mpangamila , wamsema tukio hilo limetokea baada ya baba wa mtoto huyo kumvamia mtoto wake nyakati za usiku wakati akiwa amelewa kwa kumpiga na ngumi na mateke na kupelekea kufariki dunia.
wamesema kufuatia kipigo hicho waliamua kumkimbiza kwenye kituo cha afya matai ambako aliweza kufariki dunia na kuwa licha ya mtoto wake kupigwa lakini hata yeye kama mama mzazi alipigwa vikari na kuwa tukio hilo lilitokea wakati mumewe akiwa amelewa vibaya.
Rafael Sinyangwe ambae ni mwenyekiti wa kijiji hicho, amebainisha kuwa hilo ni tukio la tatu kwa mtuhumiwa huyo kwani amekuwa akiwapiga ndgu zake kila wakati na kufikia hatua nya kufanya mauaji dhidi ya mtoto wake.
Diwani wa kata hiyo Lejiusi Boimanda amemtaja mtuhumiwa kuwa ni pyusi Salimu na kulani vikali kitendo hicho na kuishauri jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkoanoni.
Katibu tarafa ya matai Endru Manyema Ngindo , amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema jeshi la polis wilayani humo lilifika eneo la tukio na mtuhumiwa ambae ni baba mzazi wa marehemu amekamatwa .
Written By Peter kapola.

0 comments:
Post a Comment