Mwandishi wa habari wa Gazeti la Uhuru, Mariam Mziwanda, amejeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu, eneo la Tabata TOT jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo baada ya gari dogo alilokuwa akiliendesha lenye namba za usajili T222 DJX kugongana na lori la mizigo lenye namba za usajili T 495 na kisha kuingia katikati na kubanwa na lori la mafuta lenye namba za usajili T 748 BMT.
Kwa mujibu wa dereva wa lori la mafuta lililohusika katika ajali, William Colonel, chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa lori la mzigo ambalo liliacha njia na kupanda kingo za katikati ya barabara, kisha kupinduka na kuangukia lori la mafuta na gari lililokuwa likiendeshwa na Mziwanda.
Lori la mafuta na gari dogo yote yalikuwa upande wa kushoto wa barabara. Imeelezwa lori hilo baada ya kuanguka lililibana gari dogo lililokuwa katikati.
Shuhuda wa ajali hiyo, Adeodatus Sylivester Charles "Nilimtambua majeruhi kwani namfahamu tangu akiwa mtoto na sasa ni mwandishi wa habari wa Gazeti la Uhuru" amesema shuhuda Huyo.
Anasema baada ya ajali kutokea alikuta wasamaria wema tayari wanamtoa majeruhi kwenye gari akiwa ameumia sana.
“Nilikuta ametolewa kwenye gari yake akiwa ameumia sana, nikamsaidia kuvitoa vitu vyake kama simu na pochi na kumpelekea maana alikua analalamika simu yangu simu yangu, na watu walikua tayari wameshasogea eneo la ajali wanagombania vitu hivyo.
Madereva wote wa malori walitoka salama bila majeraha ya aina yoyote.
KAPOLANEWZ.
0 comments:
Post a Comment