Watu wanne wamefariki dunia papo hapo huku wengine 19 wakijeruhiwa baada ya basi ndogo la abiria aina ya Coaster walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori la kokoto jana usiku.
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa alisema ajali hiyo ilitokea katika kijiji cha Chamakweza kata ya Vigwaza Chalinze mkoani Pwani.
Alisema kati ya waliofariki yumo pia dereva wa basi hilo na majeruhi 19 saba kati yao hali zao mbaya na 12 wamepata majeraha madogo madogo.
"Costa ilikua inakwenda Mbezi na imegongana uso kwa uso na lori la kokoto na kusababisha vifo vya watu wanne.”
“Majeruhi saba wana hali mbaya wana majeraha makubwa na zaidi na 12 wameumia lakini wana afadhali tofauti na hao saba na wote wanapatia matibabu katika kituo cha afya Chalinze," alisema Nyigesa.
0 comments:
Post a Comment