Mwanafunzi wa darasa kwanza katika Shule ya Msingi Seliani, wilayani Arumeru mkoani Arusha, Emanuel Zakaria (7), amenusurika kufa baada ya kutumbukia ndani ya choo cha
shimo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng’azi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo jana wakati mwanafunzi huyo alipokwenda kujisaidia wakati wa mapumziko.
“Tunaangalia chanzo cha kuvunjika kwa shimo hilo ni nini na
ukizingatia sasa hivi ni kipindi cha mvua kubwa zinazoendelea
kunyesha, tutaangalia pia kama ujenzi haukuwa madhubuti au ni
kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha bado tunafanya uchunguzi wa
tukio hilo,” alisema.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro, alisema tukio hilo lilitokea
majira ya saa 3: 45 asubuhi muda mfupi kabla ya muda wa mapumziko.
Alisema mwanafunzi huyo, mkazi wa Kijiji cha Olevolosi, baada ya kuopolewa, alipelekwa kwenda kupata matibabu katika Hospitali ya Selian na kwamba hali yake
inaendelea vizuri.
Muro alisema lilitokana na kutitia kwa ardhi
kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali ya mkoani
Arusha.
Mkuu huyo wa wilaya aliwapongeza wananchi wa eneo hilo kwa utayari na kutoa kwa moyohali ambayo ilisaidia kunusuru maisha ya mwanafunzi huyo.
“Niwapongeze wananchi kwa utayari wa moyo wenu wa kujitolea, serikali
inataka watu wenye moyo wa kujitolea kama walivyofanya leo (jana)
kuokoa maisha ya mwanafunzi huyu,” alisema.
Hata hivyo, alisema Serikali ipo tayari kuungana na wananchi katika
ujenzi wa choo cha kisasa hadi kitakapokamilika.
“Nimeshatoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Arusha, waanze mchakato wa ujenzi wa choo kipya, Jumatatu, nitakuwa
shuleni hapo kushirikiana nao ili kuhakikisha ujenzi huo
unakamilika kwa wakati,” alisema.
0 comments:
Post a Comment