Friday, November 2, 2018 Mke wa Mchungaji Akutwa Amejinyonga Kanisani


Mke wa Mchungaji wa Kanisa la Last Church, Rusajo Mwambene (40), amekutwa amekufa kwa kujinyonga kwa kamba ndani ya kanisa hilo, katika Kijiji cha Shilinga Kata ya Ngulilo wilayani Ileje mkoani Songwe.

Selina Kayange, mkazi wa Ileje, alisema mwanamke huyo alikuwa na mtoto mchanga, ambaye alifariki dunia siku chache zilizopita.

Selina alieleza kuwa tangu kufariki dunia kwa mtoto huyo, mwanamke huyo alibadilika na alikuwa akienda makaburini kulia na baadaye hakuonekana nyumbani.

Alisema baada ya kutoonekana, waumini walipoingia katika kanisa hilo kwa ajili ya kufanya ibada, walimkuta akining’inia juu ya dari akiwa ameshakufa kwa kujinyonga kwa kamba.

Alisema hali hiyo ilizua taharuki kwa wakazi wa eneo hilo na wilaya kwa ujumla.

“Kitendo cha kuchukua maamuzi magumu ya kujiua kimeushangaza umma kutokana na kuwa ni mke wa mchungaji, lakini tumeshirikiana na viongozi kuuzika mwili huo baada ya uchunguzi wa kipolisi na kitabibu kukamilika,’’ alisema Kayange.

Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, Nickodemus Yanga, jana alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo, na kusema alipata taarifa kutoka kwenye uongozi wa kijiji kisha alitoa taarifa kwa viongozi wa wilaya ambao walifika katika eneo hilo kwa ajili ya uchunguzi.
Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment