Wito umetolewa kwa wananchi mkoani Morogoro kushiriki katika maadhimisho ya siku ya wazee duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo October mosi ikiwa na lengo la kutetea haki za wazee pamoja na boresha maisha yao.
Wito huo umetolewa na mkurugenzi msimamizi wa shirika la Helpage International Bwana Smart Emmanuel wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Kipepeo uliopo hoteli ya Savoy mkoani humo.
Sambamba na hayo Mkurugenzi huyo amesema kuwa maadhimisho ya mwaka huu yatakuwa tofauti na miaka iliyopita kwani yatashirikisha ngazi ya kijiji, ngazi ya kata, wilaya, hata mikoa kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali kama vile taasisi za dini pamoja na vyuo vya elimu ya juu kwa ajili ya kutoa maarifa kutokana na taaluma zao.
Hata hivyo bwana emmanuel amebainisha changanoto zinazowakabili wazee kwasasa ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa huduma za afya, kudhurumiwa haki zao kama vile mauaji,kukosa makazi , ugomvi wa ardhi, kutokupata kipato cha uhakika na kukosekana kwa sheria kwa ajili ya kulinda haki za wazee
Aidha amesema kuwa Maadhimisho hayo yalianza kuadhimishwa rasmi mwaka 1991, ambapo kitaifa mwaka huu yatafanyikia mkoani mtwara yakisindikizwa na kauli mbiu isemayo “ KUIMARISHA USAWA KUELEKEA MAISHA YA UZEENI”.
NA PETER KAPOLA MOROGORO 0755747892
0 comments:
Post a Comment