March 28,2019.
Rukwa-kalambo
Mtu mmoja mkazi wa kijiji na kata ya Mkoe wilaya ya kalambo mkoani Rukwa Girubat lungwa miaka 34 amefariki dunia baada ya radi kubomoa ukuta wa nyumba yake kisha kuingia ndani na kusabisha kifo chake hapo papo.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea kufuatia mvua kubwa iliokuwa imeambatana na upepo mkali kunyesha maeneo hayo kisha kusababisha kifo cha mtu moja na mmoja kujeruhiwa wote ndugu wa familia moja.
Awali kisimulia mkasa huo mwenyekiti wa kijiji hicho Joseph Machipa amesema radi hiyo ilijikeza kijijini hapo na kuingia ndani ya nyumba ya mwananchi wake kupitia kona ya nyumba yake ambapo kabla ya kuingia ilichoma mifugo yake ikiwemo mbuzi watatu ,kuku na mbwa mmoja.
Amesema baada ya kifo cha kijana huyo ili mfata kaka mtu na kumjeruhi vibaya .
Ievocatus lungwa ni mmoja wa wathirika wa tukio hilo, amesema radi hiyo ilimpiga mara baada ya kusabisha maafa ya kaka yake.
Kaimu mtendaji wa kata hiyo Noel Kaduma amekili kutokea kwa tukio hilo na kusema tukio ni lapili kutokea katika maeneo hayo.
Hali hiyo imemlazimu Kaimu mkurugenzi wa halmashuri hiyo jabiri Ally kufika eneo la tukio na kuwapa pole wathirika wa tukio hilo.
Na Mwandishi wa Habari Peter kapola Rukwa 0755747892
0 comments:
Post a Comment