Jeshi la
Polisi kikosi cha usalama barabarani mkoani RUKWA limezindua
kongamano la usalama barabarani ili kuendesha zoezi la kukagua vyombo vya
moto na kutoa elimu ya kuzuia ajali zinazotokana na uzembe
Mkuu wa
kikosi cha usalama barabarani mkoa wa RUKWA,mrakibu msaidizi WENSESLAUS
GUMHA amesema zoezi hilo litawataka waendeshaji wa vyombo vya moto
kutii sheria bila shuruti ya kukaguliwa vyombo vyao kabla ya msako wa
kuwabaini watakaochelewa kufanya hivyo
Amesema
lengo la zoezi hili la ukaguzi na kukabiliana na ajali zinazosababishwa na
vyombo vya moto visivyokuwa na sifa ya kutoa huduma barabarani
INSERT - MRAKIBU
MSAIDIZI WENSESLAUS GUMHA-MKUU WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI RUKWA
Mgeni rasmi
wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kongamano la usalama barabarani mkoa
wa RUKWA kamanda wa jeshi la Polisi mkoani humo kamishna
msaidizi wa Polisi MATHIAS NYANGE ametoa wito kwa madereva wa
vyombo vya moto kushiriki kongamano hili kauli inayoungwa mkono na baadhi ya
wadau wa usalama barabarani
INSERT -KAMISHANA MSAIDIZI MATHIAS NYANGE-KAMANDA WA
POLISI MKOA WA RUKWA -KASIANI KAEGELE-MWENYEKITI WA KONGAMANO -ATHUMAN OMARI-AFISA MWANDAMIZI WA
SUMATRA-RUKWA -ROGETHA
BAMOTO-KATIBU WA MADEREVA
Imeelezwa
hatua hii ya ukaguzi wa vyombo vya usalama barabarani itasaidia kupunguza ajali
zinazotokana na ubovu wa vyombo hivyo
0 comments:
Post a Comment