Moshi. Wanafunzi wawili wa Shule ya Sekondari Kisomachi, iliyopo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wamefariki dunia baada ya kudaiwa kukosa hewa, wakati walipoingia kwenye pipa la kuhifadhia maharage.
Akizungumza Mwenyekiti wa Kijiji cha Kileuwo wilayani hapa, Godfrey Mrema amesema tukio hilo limetokea Mei 12, 2023, wakati wanafunzi hao walipoingia kwenye pipa hilo kwa ajili ya kutoa maharage ya chakula shuleni.
0 comments:
Post a Comment