#HABARI Waziri wa Maliasili Mohamed Mchengerwa na RC Mbeya wamefika Kijiji cha Mwanavala wilayani Mbarali kutokana na agizo la Waziri Mkuu la kuwataka kufika ili kuona hali ya ugomvi uliotokea baina ya wananchi na Askari wa TANAPA na kubaini hakuna vifo wala mifugo iliyoshikiliwa wala ng'ombe waliouawa.
Hoja hiyo ya vurugu kati ya wananchi na wahifadhi wa TANAPA iliibuliwa na Mbunge wa Mbarali, Fransis Mtega, aliyeomba kutoa hoja ya dharura ya kulitaka Bunge lijadili suala hilo na ndipo @kassim_m_majaliwa alipotoa maelekezo.
"Nimesikitishwa na kauli za Mbunge malalamiko na shutuma zake zimeleta taharuki ambayo sijaikuta eneo hili na wananchi wamekiri kuingia ndani ya eneo hili na wameiomba serikali kuharakisha mchakato wa kuwatafutia maeneo ya kuishi" amesema Waziri Mchengerwa
#kapolanewsupdates
0 comments:
Post a Comment