Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Kangi Lugola ameagiza kampuni 7 zilizohusika katika ubadhilifu wa fedha katika zabuni ya kununua mfumo wa kusajili watu wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA kufika ofisini kwake Agost 3 mwaka huu wakiwa na fedha mkononi.
Kangi anatoa maagizo hayo July 25, 2018 akiwa mkoani Dodoma muda mfupi baada ya kumaliza mazungumzo na kampini ya IRIS COPERATION iliyopewa zabuni ya kuleta mtambo wa kutengeneza vitambulisho ghafi vya taifa ambayo haikuleta mtambo huo kwa miaka mitatu hadi sasa.
Aida Waziri Kangi Lugola amemtaka aliyekuwa Mkurugenzi wa NIDA Dicksin Maimu kuripoti ofisini kwake siku hiyo na maelezo juu ya ubadhilifu uliojitokeza ili maamuzi yaweze kutolewa kwani hakuna mtu aliyafanya ubadhilifu atakayebaki salama
“Kuna ufisadi ndani ya NIDA na kwamba wale wote wanaojijua walijihusisha na ufisadi wa fedha za umma siku zao zinahesabika na ninatoa salamu kwao kwamba hawatasalimika na wafanye maamuzi ya kufika ofisini kwangu tarehe 3 mwezi wa nane mwaka huu” –Waziri Kangi Lugola.
0 comments:
Post a Comment