Tuesday, August 28, 2018 CHADEMA Washinda unaibu Meya Arusha


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (chadema) jijini Arusha kimeshinda nafasi ya naibu meya wa Jiji baada ya mgombea wake Paulo Matthysen kumbwaga mgombea wa CCM, Prosper Msofe.

Uchaguzi huo uliofanyika jana baada ya kuapishwa kwa madiwani wanne wa CCM, ambao awali wote walikuwa ni wanacahama wa Chadema ni pamoja na Matthysen ambaye ni diwani wa Mushono amepata kura 27 za madiwani wote wa chadema  na Msofe ambaye ni diwani wa Daraja mbili amepata kura saba za madiwani wote wa CCM katika baraza hilo.

Akitangaza  matokeo hayo, Mwanasheria wa jiji, Grayson Orcado alisema wapigakura halali katika uchaguzi huo walikuwa  34 na hakuna kura  iliyoharibika.

Akizungumza baada ya kutangazwa kwa matokeo, Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro alisema ushindi huo umedhihirisha kuwa madiwani wa chama hicho bado wako imara jijini humo.

“Ushindi huu unaonyesha bado tupo imara, lakini pia leo tumempokea mkurugenzi mpya, Dk Maulid Madeni aliyeteuliwa na Rais John Magufuli, tunaahidi kumpa ushirikiano wa kutosha,” alisema meya huyo.

Alisema kikao hicho ambacho ni cha robo ya nne ya mwaka, kimewachaguwa pia wenyeviti wa kamati wote kutoka chadema.

Meya Lazaro amesema Diwani wa Sombetini, Ally Benanga alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya mipango miji na diwani wa Ngarenaro, Isaya Doita alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya elimu, afya na uchumi.

Wakati huo huo, kabla ya uchaguzi huo, madiwani wanne wa CCM walioshinda katika uchaguzi wa Agosti 12 waliapishwa jana. Madiwani hao ni Msofe wa Daraja mbili, Emmanuel Kessy wa Kaloleni, Obedi Meng'oriki wa Terati na Elirehema Nnko  wa Kata ya Osunyai .
Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment