Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limesema litaomba vyombo vya kutunga sheria kuondoa biashara ya bodaboda, kufuatia madereva wa vyombo hivyo kutotii magizo mbalimbali ya serikali ikiwemo la kuwataka kila mwendesha bodaboda kuwa na kofia ngumu mbili.
Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Gemini Mushy kufuatia agizo la Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme alilolitoa mwezi mmoja na nusu uliopita wa kuwataka madereva wa bodaboda kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja wanakuwa na kofia ngumu mbili, jambo ambalo bodaboda wanaonekana wameshindwa kulitekeleza huku wakitoa sababu mbalimbali.
Mbali na Kamanda huyo kusema hivyo nao baadhi ya abiria wa bodaboda mkoani humo wamesema, hata wao wangependa kuvaa kofia hizo lakini linapofika suala la kudai kofia, madereva bodaboda hao hutoa sababu zisizo na msingi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma amesema wamechukua hatua mbalimbali za kuwakamata baadhi ya madereva bodaboda kuwaweka ndani na kuwafikisha mahakamani lakini bado wamekuwa wagumu kutii bila shuruti.
0 comments:
Post a Comment