Mkazi wa Makumbusho Dar es Salaam, Said Mussa, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa tuhuma za kubaka.
Mwendesha Mashtaka, Credo Rugaju alidai mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Anifa Mwingira kuwa katika tarehe isiyofahamika mwaka huu eneo la Makumbusho, alimbaka binti wa miaka 16 (Jina limehifadhiwa).
Mshtakiwa alikana mashitaka na alishindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo alirudushwa rumande hadi Septemba 4 mwaka huu kesi itakapotajwa tena.
0 comments:
Post a Comment