Tuesday, January 1, 2019 Mwanamke Auawa Kikatili......Mwili wake wafungiwa ndani ya banda la ng'ombe Mkoani Katavi


Mkazi wa  Kijiji cha Luhega, Wilaya ya Tanganyika, Milembe  Manoni (22), amekutwa ameuawa kwa kuchomwa na kisu kifuani, kisha mwili wake kufungiwa ndani banda ng’ombe.

Akizungumzia tukio hilo jana,  kaka wa  marehemu, Nestory Malongo  alisema lilitokea  juzi usiku nyumbani kwa marehemu.

Alisema taarifa ya kuuawa kwa  Milembe aliipata  saa tatu  asubuhi na wasamalia wema,

Baada ya kapata taarifa hizo, alikwenda eneo la tukoo na kukuta watu wengi wakiwa wamekusanyika nje ya nyumba.

Alisema baada ya kuona mwili hiyo, waliona majereha sehemu za kifuani ambayo inaonyesha alichowa na kisu.

Alisema polisi  walifika eneo hilo, kisha kuuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya kwenda kuufanyia uchunguzi Hospitali ya Rufaa ya  Mkoa wa  Katavi .

Mama wa marehemu,  Tuma Matine alisema alipigiwa simu na mkwe wake na kusisitiza kitendo hicho ni cha kikatili mno.

 Alisema  katika  nyumba hiyo, binti yake alikuwa kuwa akiishi na mfanyakazi mmoja ambaye alikuwa akifanya kazi ya kuchunga  mifugo ya ng’ombe.

“Nasikitika baada ya tukio hili huyu mfanyakazi hajaonekana nyumbani…inawezekana wazi ndiye aliyehusika na kifo hiki,”alisema.

Mwenyekiti wa chama cha wafugaji wa mifugo wa  Mkoa wa  Katavi, Mussa Kabushi  alisema kumekuwapo na mauaji ya mara kwa mara ya kuuawa kwa wafugaji.

Alisema mauaji hayo, yamekuwa yakisababishwa kutokana na tabia ya wafugaji kukaa kwenye maeneo ya kujitenga na kutokuwa na ulinzi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Damas  Nyanda alithibitisha kutokea kwa mauaji  hayo na kusema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi.
Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment