Mkazi mmoja
mkoani RUKWA anayejishughulisha na kilimo cha mazao ya chakula
na biashara CHRISANT MZINDAKAYA amewataka wakulima wa
zao la mahindi mkoani Rukwa kuendelea kulima zao hilo licha ya changamoto
zilizojitokeza katika msimu uliopita wa kilimo
MZINDAKAYA ameieleza Chemchemi radio kuwa
baadhi ya wakulima wa zao la mahindi mkoani RUKWA wameamua kulima mazao
mengine ya maharage na alizeti katika msimu wa kilimo wa mwaka 2018/19
baada ya kuanguka kwa bei ya zao la mahindi katika msimu uliopita wa kilimo
Amesema
kilimo cha mahindi bado ni muhimu kwa ajili ya hifadhi ya chakula na pia kwa
ajili ya usindikaji wa viwanda vya nafaka na kusema ukosefu wa soko la uhakika
wa zao la mahindi hauwezi kuondoa umuhimu wa mahindi kuufanya mkoa wa RUKWA kuwa
na sifa ya ulimaji wa zao hilo kwa uwingi hapa nchini
Ushauri wa
mkulima huyu unafuatia kauli za baadhi ya wakulima mkoani RUKWA wakati
wakiongea na Chemchemi radio kuelezea sababu zilizosababisha
baadhi ya wakulima kulima mazao mengine badala ya mahindi kufuatia changamoto
ya soko iliyojitikeza katika msimu uliopita wa kilimo
Msimu wa
kilimo kwa mwaka 2018/19 umeanza katika maeneo mengi ya mkoa wa RUKWA huku
baadhi ya wakulima wakionyesha nia ya kupunguza kiwango cha ulimaji wa zao la
mahindi kutokana na changamoto ya soko la uhakika.
0 comments:
Post a Comment