Jumla ya vijana 67 wamepata sakramenti ya kipaimara tayari kuwa wafuasi na askari hodari wa yesu kristu kwa kuishuhudia na kuitangaza imani ya kanisa katoliki ulimwenguni kote .
Sakramenti hiyo imetolewa na Mhashamu Askofu Telesphor Richard Mkude wa jimbo katoliki morogoro wakati wa sadaka ya adhimisho la misa takatifu ya uzinduzi wa kigango cha mtakatifu Fransisko wa sales kilichopo lukobe parokia ya matakatifu monika kihonda jumapili ya 4 mwaka c wa kanisa misa iliyoambatana na utoaji wa sakramenti ya kipaimara.
Akizungumza katika homilia yake kwa waimarishwa hao pamoja na waamini walioshiriki katika adhimisho hilo amewaasa kuyashika na kuyafuata mafundisho ya kikristu ambayo yana ukweli ndani yake ambao unatoa uzima wa milele hatimae utakatifu.
Akitolea mfano wa simu yenye chaji Askofu mkude amesema kuwa mkristu anapo hudhuria katika ibada na misa takatifu anaongeza uchaji wa imani ,matuimani na mapendo kwa mwenyezi mungu .
Kwa upande wake padre Ireneus Mwinuka mzawa wa kutoka shirika la bikira maria wa mlima Karmeli Kihonda maghorofani amewataka wazazi na walezi kuwa nguzo ya kanisa kwa kuwahimiza watoto na vijana kujiunga na miito mitakatifu wa utawa na upadre ili kanisa liweze kutoa huduma ya uinjilishaji.
Misa hiyo ilihudhuriwa na Paroko wa parokia ya mtakatifu monika Padre Octavian msimbe ,mlezi wa kigango hicho Padre Nelson Antony wa shirika la mtakatifu fransisko wa sales kihonda, padre Irneus Mwinuka mzaliwa wa kata ya lukobe kutoka shirika la bikira maria wa mlima karmeli kihonda shemasi piense severine punguti,Masista wa shirika la maria imakulata kihonda na viongozi mbali mbali wa serikali kata ya lukobe.
NA PETER KAPOLA MOROGORO.
0 comments:
Post a Comment