Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kambi ya Tabora, Esther Gway amefariki wakati akijiokoa katika tukio la ubakaji lililotekelezwa na kijana aliyedaiwa kuwa ni fundi ujenzi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora, Emmanuel Nley amesema tukio hilo limetokea juzi Jumapili Januari 27, 2019 saa moja usiku katika eneo la Kariakoo mjini humo.
Kamanda Nley amesema kwamba mtuhumiwa alimvizia mwanajeshi huyo akiwa nyumbani kwake muda huo na kumkaba shingo kisha kumuangusha chini na katika purukushani za kutaka kumbaka huku akimkaba shingoni alisababisha kifo chake.
"Fundi huyo inadaiwa alikuwa akijenga nyumba ya marehemu eneo la Kariakoo katika manispaa ya Tabora, tayari anashikiliwa na Jeshi la Polisi na tunaendelea na uchunguzi, tayari mwili wa marehemu upo katika uchunguzi pia hospitalini", amesema Kamanda Nley.
Akizungumzia taratibu za maziko ya marehemu amesema kuwa baada ya uchunguzi, mwili wa marehemu utakabidhiwa kwa ndugu pamoja na Jeshi ili taratibu za mazishi ziendelee.
0 comments:
Post a Comment