Ni jambo unaloweza kuliita ni ajabu ambapo mtoto wa umri wa mwezi mmoja
tangu kuzaliwa kuota meno saba na kusababisha Madaktari kumfanyia
upasuaji kuyaondoa meno hayo.
Tukio hilo limetokea India ambapo mmoja wa Madaktari waliomfanyia
upasuaji mtoto huyo, Meet Ramatri amesema upasuaji umekuwa na mafanikio
baada ya kufanyiwa upasuaji mara mbili; upasuaji wa kwanza ulikua wa
kutoa kwanza meno manne na baadaye akatolewa meno matatu.
Wazazi wa mtoto huyo waligundua kuwa mtoto wao hanyonyi vizuri hivyo
kuamua kumpeleka Hospitali ili kufanyiwa uchunguzi ndipo madaktari
walipogundua mtoto huyo ana tatizo hilo ambapo hata hivyo daktari huyo
ameeleza haijulikani kama upasuaji huo utaathiri uotaji wa meno wa mtoto
huyo kwa siku za usoni.
0 comments:
Post a Comment