Mbunge
wa Rombo, Joseph Selasini ameeleza jinsi Mbunge wa Singida Mashariki,
Tundu Lissu alivyopigwa risasi nyumbani kwake mjini Dodoma.
Selasini
amesema kuwa maelezo aliyopata ni kuwa alikuwa akifuatiliwa na gari
tangu anatoka bungeni na dereva wake alilishtukia.
Amesema kuwa alivyoona wanamfutilia alipofika nyumbani, dereva alimsihi Lissu asishuke ndani ya gari.
"Hao
watu walipoona hawashuki walijifanya kuna kitu wanaangalia walivyoona
kuna utulivu walisogeza gari lao ambalo ni tinted na kuanza kurusha
risasi upande wa Lissu." amesema
Selasini amesema, “Risasi zilimpata mguuni, mkononi na tumboni lakini daktari anasema anaendelea vizuri."
Lissu amepigwa risasi leo Alhamisi na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.
0 comments:
Post a Comment