Jeshi
la polisi mkoani Dodoma limeagiza Dereva wa Tundu Lissu kujisalimisha
Polisi haraka iwezekanavyo kwa ajili ya uchunguzi wa awali kuhusiana na
tukio la mbunge wa Singida Mashariki,mwanasheria mkuu wa CHADEMA na rais
wa TLS,Tundu Lissu kupigwa risasi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo,Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amemtaka dereva huyo ajisalimishe polisi.
"Polisi
inamtaka dereva wa Tundu lissu ajitokeze na afike Polisi Dodoma bila
kukosa au makao makuu ya upelelezi Dar es salaam ili aweze kutoa
maelezo”,alisema Muroto
“Kutoweka
kwake na kujificha ni kosa la jinai na kama kuna mtu au watu wanamficha
wanatenda kosa la jinai, wamfikishe Polisi bila kukosa kwa kuwa ni
shahidi muhimu katika upelelezi”,aliongeza Muroto.
Aidha
asema magari 8 pia yamekamatwa aina ya Nissan na Watuhumiwa wanaendelea
kuhojiwa ili kubaini ni kina nani wamefanya shambulizi hilo kwa Tundu
Lissu ambapo Jeshi la Polisi bado linaendelea kutoa wito kwa Wananchi
wenye taarifa za tukio hilo waendelee kuzifikisha Polisi.
0 comments:
Post a Comment