Mbunge
wa Iringa Mjini (CHADEMA) Mchugaji Peter Msigwa amefunguka na kuonyesha
kutoridhishwa na kauli ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon
Nyakoro Sirro kusema Tundu Lissu hakuwahi kutoa taarifa juu ya watu
wanaomfuatilia.
Mbunge
Msingwa ambaye sasa yupo nchini Kenya kwenye matibabu ya Tundu Lissu
ameonyesha kusikitiswa na taarifa hiyo ya IGP ambayo aliitoa Septemba 8,
2017 katika mkutano wa waandishi wa habari na kusema kiongozi huyo
hakuwahi kutoa taarifa yoyote polisi juu ya gari ambalo lilikuwa
likimfuatilia kabla ya kupatwa na shambulizi hilo la kupigwa risasi.
"Kamanda
Sirro Ulitaka Lissu atoe taarifa gani zaidi? Sisi wengine ni wanasiasa,
hatuna mafunzo ya kijeshi, Polisi wala Kikachero. Silaha yetu kubwa ni
kipaza sauti (microphone), kazi yetu ni kupaza sauti , hoja inapaswa
kujibiwa kwa hoja! Siyo kwa mabomu ya machozi, sio kwa virungu na
bunduki. Inaonyesha jeshi letu la polisi uwezo wake mkubwa ni kupambana
na vyama vya siasa hasa CHADEMA na CUF kuwalinda wakuu wa wilaya na
mikoa" aliandika Mchungaji Msigwa
Aidha
Msigwa anasema anaumia kuona Tundu Lissu akiteseka kwa ajili ya kutetea
haki na Demokrasia ya taifa la Tanzania na kusema alichofanyiwa Tundu
Lissu kinampa ujasiri wa kusonga mbele.
"Mungu
anakataza kumwaga damu isiyo na hatia! machozi yanitoka kuona rafiki
yangu Tundu Lissu akiteseka kwa kutetea haki na demokrasia ya taifa
letu, amewakosea nini? Inanipa ujasiri wa kusonga mbele, sitanyamaza,
tunakupenda Lissu wewe ndiye shujaa wetu" aliandika Msigwa
0 comments:
Post a Comment