Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu
akiendelea kupatiwa matibabu baada ya kupigwa Risasi hii leo mkoani
Dodooma (Picha na Mwananchi Digital)
****
Mbunge wa Singida Mashariki, ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, na rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)Tundu Lissu leo mchana Alhamis Septemba 7,2017 amepigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa Dodoma na inaelezwa kuwa hali yake ni mbaya.
Tundu Lissu amepelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano,
Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema Mh. Lissu
amepigwa risasi zaidi ya mbili alipokuwa ametoka bungeni na kwenda
nyumbani kwake kwa ajili ya chakula cha mchana.
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani
Bungeni, Freeman Mbowe, wabunge na viongozi wengine wa ulinzi wa Bunge
wamefika katika hospitali hiyo kujua kinachoendelea.
Akizungumza na kituo cha ITV Mwenyekiti wa CHADEMA Freeaman Mbowe amesema "Hali ya Tundu Lisu ni mbaya Sana, na msishangae mkasikia lolote kuanzia sasa"
Baadhi ya ndugu na wagonjwa wamefurika katika chumba cha upasuaji cha hospitali ya mkoa wakitafakari, huku wengine wakilia.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Charles Kihologwe amewataka watu hao
kukaa mbali na chumba cha upasuaji lakini wengi wanakataa wakisema
hawamwamini mtu yeyote.
Asubuhi, Lissu alihudhuria kikao cha Bunge na aliomba mwongozo wa Naibu
Spika akihoji kuhusu taarifa za kamati zilizoundwa na Spika wa Bunge,
Job Ndugai kutathmini mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti
wa madini ya Tanzanite na almasi kuwasilishwa kwa Waziri Mkuu badala ya
kujadiliwa na Bunge kwanza.
Mbowe akiwa na Dereva wa Tundu Lissu aliyeshika nguo zenye damu
Dereva wa Tundu Lissu
Gari la Tundu Lissu alilokuwa nalo
Matundu ya risasi katika gari
0 comments:
Post a Comment