Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe amesema Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu
Lissu amepigwa risasi leo Alhamisi nyumbani kwake na kwamba hali yake ni
mbaya.
Lissu, ambaye ni mwanasheria mkuu wa Chadema kwa sasa amepelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.
Katibu
wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, wabunge na viongozi wengine wa ulinzi
wa Bunge wamefika katika hospitali hiyo kujua kinachoendelea.
Baadhi ya ndugu na wagonjwa wamefurika katika chumba cha upasuaji cha hospitali ya mkoa wakitafakari, huku wengine wakilia.
Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Charles Kihologwe amewataka watu hao kukaa
mbali na chumba cha upasuaji lakini wengi wanakataa wakisema hawamwamini
mtu yeyote.
Asubuhi,
Lissu alihudhuria kikao cha Bunge na aliomba mwongozo wa Naibu Spika
akihoji kuhusu taarifa za kamati zilizoundwa na Spika wa Bunge, Job
Ndugai kutathmini mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa
madini ya Tanzanite na almasi kuwasilishwa kwa Waziri Mkuu badala ya
kujadiliwa na Bunge kwanza.
0 comments:
Post a Comment