IGP
Simon Sirro amefunguka na kusema kuwa viongozi wastaafu wa jeshi la
polisi nchini wamempa ushauri namna ambavyo anapaswa kuendesha jeshi
hilo na kudai viongozi hao wameona mapungufu mbalimbali ndani ya jeshi
hilo ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi.
Akiongea
na waandishi wa habari IGP Sirro jana baada ya kumaliza mkutano na
wastaafu hao alisema mambo kadhaa ambayo alishauriwa na viongozi hao
ambayo jeshi la polisi linatakiwa kulifanyia kazi.
"Jambo
kubwa ambalo walikuwa wanasisitiza ni suala la weledi kwamba wanapokuwa
kule wanatuangalia sisi ambao tuko jeshini tunahudumia Watanzania
wanaona kuna mapungufu katika baadhi ya utendaji wa askari wetu, kwa
hiyo walikuwa wanasisitiza sana katika suala la weledi, lakini la pili
viongozi hawa wanazungumzia sana suala la mafunzo kwamba kila askari
anapaswa kuwa na mafunzo mbalimbali" alisema IGP Sirro
Baadhi
ya maafisa wastaafu wa jeshi la polisi walioshiriki katika kikao hicho
ni pamoja na IGP Mstaafu Ernest Mangu, saima Mwema, Omari Maita pamoja
na makamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleman Kova na
Afred Tibaigana
0 comments:
Post a Comment