Thursday, March 8, 2018 Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) aliyetoweka Apatikana Mafinga Akiwa Ametupwa


Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania , Abdul Nondo ambaye pia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) aliyeripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha amepatikana akiwa hai eneo la Mafinga mkoani Iringa.

Imeelezwa kuwa, Nondo alijikuta katika eneo hilo baada ya kuzinduka kutoka katika lindi la usingizi na kuwauliza wenyeji wa eneo hilo kuwa hapo ni wapi? Wenyeji hao walimfahamisha kuwa yuko Mafinga mkoani Iringa na kisha akapelekwa katika kituo cha polisi kilichoko karibu.

Polisi walifanya mahojiano na mwanafunzi huyo ili kuweza kujua nini hasa kilitoka na baada ya hapo kupiga simu kwa ndugu zake.

Baada ya Baba mzazi, Mussa Mitumba kupata taarifa za kuonekana kwa mwanae, aliomba namba za askari aliyemfanyia mahojiano ili kujua nini kilimpata mwanae aweze kujua kama jambo jingine alilowaambia kuhusiana na kupotea kwake.

Awali kabla ya tukio hilo mwanafunzi huyo alielezea kwamba alikuwa akifuatiliwa mara kadhaa watu asiowatambua.
Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment