Saturday, March 3, 2018 Marekani Yazungumzia Vitisho vya Urusi .......Ni Baada ya Putin Kutangaza Kombora Jipya Linaloweza Kutua Popote


Marekani imepuuzia mbali mtiririko wa madai yaliotolewa na Rais wa Urusi Vladimir Putin kuwa ana mkusanyiko wa mkakati wa silaha mpya za nyuklia ambazo zinaweza kupiga eneo lolote duniani.

Ikulu ya White House na Wizara ya Ulinzi zimetupilia mbali Alhamisi kauli hizo na kuziita ni za kisiasa, wakisema jaribio la Russia kuboresha nguvu zake za nyuklia limekuja bila kushangaza na haliwezi kuibabaisha Marekani.

“Rais Putin amethibitisha kile ambacho Marekani imekuwa ikikijua kwa muda mrefu,” msemaji wa ikulu ya White House Sarah Huckabee Sanders amesema.

Russia imekuwa ikitengeneza mifumo yenye kusudio la kudhoofisha silaha kwa zaidi ya muongo mmoja ikikiuka moja kwa moja majukumu yake yaliyoko katika makubaliano.

“Marekani inaendelea kuboresha vichwa vya silaha za nyuklia viwe vya kisasa zaidi na kuhakikisha kuwa uwezo wetu haulingani na yoyote,” ameongeza, akigusia bajeti mpya ya dola bilioni 700 ya jeshi la Marekani.

Maafisa wa ulinzi wa Marekani pia wamesema madai ya Russia sio mageni kabisa kwao.

“Tumekuwa tukifuatilia hatua za Russia,” msemaji mkuu wa Wizara ya Ulinzi Dana White amewaambia waandishi Alhamisi. Silaha hizi ambazo Putin anazizungumzia zimekuwa zikitengenezwa kwa muda mrefu sasa.”

“Wananchi wa Marekani watulie hali wakiwa na uhakika kuwa sisi tumejitayarisha kikamilifu,” amesema.

Rais wa Urusi Vladimir Putin Alhmisi alisema jeshi lake limejaribisha silaha kadhaa mpya za nyuklia ikiwemo aina ya kombora ambalo halina ukomo wa masafa na linaweza kupenya ngome ya mfumo wowote unaokabiliana na makombora.

Alikuwa akizungumza na wabunge katika hotuba yake ya taifa kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika Machi 18 nchini Russia. Putin atakuwa anatumikia awamu ya tatu kama rais na anatarajiwa kushinda na kuendelea kushikilia wadhifa wake kwa miaka sita.

Pamoja na kombora hilo, Putin amesema kuwa Urusi tayari imejaribisha kombora lake jipya ambalo linauwezo wa kufika katika mabara tofauti – linaloitwa Sarmat- ambalo ni la masafa marefu na lenye kubeba silaha nyingi zaidi kuliko lile la awali.
Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment