Babu aliyejulikana kwa jina la Kachuka Malongo (90) anashikiliwa na polisi mkoani Shinyanga kwa tuhuma ya kubaka wanafunzi watano wenye umri kati ya miaka 8 hadi 12 wa shule ya msingi Tinde A na B kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule amesema chanzo cha tukio hilo ni tamaa za mapenzi ambapo mtuhumiwa aliwabaka watoto hao kwa nyakati tofauti akiwarubuni kwa kuwapa pipi na pesa.
Amesema tukio hilo la wanafunzi hao kubakwa limebainika Machi 21,2018 majira ya saa 2 na nusu asubuhi
Kamanda Haule amesema wanaendelea kufanya mahojiano na mtuhumiwa na watamfikisha mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.
0 comments:
Post a Comment