Taarifa kutoka mkoani Singida ni kwamba lori la mafuta limeanguka na kuwaka moto katika eneo la Mlima Sekenke na watu wawili wameripotiwa kupoteza maisha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Deborah Magiligimba, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa watu wawili wamefariki, lakini bado hawajapata majina yao.
Magiligimba amesema kwamba, ajali hiyo imetokea saa nne na nusu asubuhi milima ya Senkenke Wilaya ya Iramba barabara ya Singida - Nzega.
Gari iliyohusika kwenye ajali hiyo ni namba T167 DTC aina ya Flight liner ambayo ilikuwa na Trailer namba T 960 ALS. Hili gari ni mali ya Petromac Africa Dar es salaam.
Gali iliacha njia na kupinduka ambapo ililipuka na kusababisha moto mkubwa uliopelekea vifo vya watu wawili ambao ni wanaume.
Uchunguzi wa jeshi la Polisi wa awali baada ya kufatilia kwenye mzani wa Singida, gari ilipimwa mzani wa Singida saa moja na dk 27 asubuhi dereva alikua anaitwa Erasto Abedi Rusazi na alikuwa na tingo msaidizi wake anayeitwa Ramadhani Hashim Ramadhini wote ni Wakazi wa Tabata Dar Es Salaam.
RPC Deborah Magiligimba, ametoa wito kwa madereva watii sharia za barabarani ili kuepusha ajali.
NA KAPOLANEWZ.
0 comments:
Post a Comment